Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Comoro: Wagombea wa upinzani wanataka matokeo ya urais kutupiliwa mbali

Kuraaa.png Comoros: Wagombea wa upinzani wanataka matokeo ya urais kutupiliwa mbali

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa upinzani katika visiwa vya Comoros wanataka matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliopita kutupilia mbali.

Wito wa viongozi hao umekuja wakati huu maofisa wa polisi wakikabiliana na waandamanaji waliokuwa wamekarishwa na kuchaguliwa tena kwa rais Azali Assoumani.

Kwa mujibu wa maofisa wa tume ya uchaguzi, Assoumani aliibuka mshindi wa uchaguzi huo baada ya kupata asilimia 62.97 ya kura zote zilizopigwa siku ya Jumapili.

Licha ya tangazo hilo la tume ya uchaguzi, wapinzani watano walioshiriki uchaguzi huo wamesema kuwa kulikwepo na udaganyifu na wizi wa kura.

Kabla ya tangazo hilo la upinzani, polisi walikuwa wamewatawanya waandamanaji kwa mabomu ya machozi walipokuwa wakijaribu kufunga barabara kwenye jiji kuu.

Msemaji wa serikali Houmed Msaidie, ametuhumu upinzani kwa kupanga maandamano hayo.

Matokeo rasimi yaliotolewa siku ya Jumanne yalionyesha kuwa Assoumani, kiongozi wa zamani wa mapinduzi ambaye baadae alikuwa rais wa kiraia, aliibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa duru ya kwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live