Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coleman afungiwa miaka mitatu

A32acf18ac8f01af432210156b1b8719.png Coleman afungiwa miaka mitatu

Thu, 29 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BINGWA wa Dunia wa mbio za mita 100, Christian Coleman amefungiwa kwa miaka miwili baada ya kukwepa kufanyiwa vipimo vya dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Mwanariadha huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 24 ambaye alifungiwa kuanzia Mei 14, mwaka huu, atakosa michezo ya Olimpiki ya Tokyo iliyoahirishwa hadi mwakani jijini Tokyo.

Coleman alishinda medali ya dhahabu ya mita 100 katika mashindano ya Dunia ya Riadha yaliyofanyika Doha, Qatar mwaka jana.

Mwakilishi wake, Emanuel Hudson amesema mwanariadha huyo anayeshikilia pia rekodi ya dunia ya mbio za ndani ya mita 60 atakata rufaa kwa Kamati ya Nidhamu wa Wanariadha (AIU) kupinga uamuzi wa Mahakama ya Michezo ya Kimataifa (Cas).

Hudson alielezea uamuzi huo kuwa ni wa bahati mbaya: "Bwana Coleman kwa sasa hana la kungea hadi wakati utakapofika,” alisema.

Coleman ambaye ni bingwa mara mbili wa dunia na ambaye ameshinda dhahabu katika mbio za kupokezana vijiti za mita 4x100 huko Doha, ana siku 30 za kuwasilisha rufaa yake.

Awali alifungiwa kwa muda tangu Juni baada ya kushindwa kufanyiwa vipimo vya mara ya tatu Desemba mwaka jana.

Chanzo: habarileo.co.tz