Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cleopatra: Ilibidi Nivue Nguo Kuthibitisha Jinsia Yangu

Cleopatra Kamburu Cleopatra Kamburu

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HII sasa ni zaidi ya udhalilishaji, mrembo Cleopatra Kamburu anasema ilikuwa aibu kutakiwa kuvua nguo zake ili kuonyesha yeye ni nani. Uganda imetoa kitambulisho cha kwanza kwa watu waliokumbatua jinsia tofauti na waliozaliwa nayo (Transgender).

Kwa neno la kiingereza ‘transgender’ ni mtu mwenye hisia tofauti na maumbile yake ya asili, kama mwanaume anakuwa na hisia za kike kama mwanamke anakuwa na hisia za kiume na wengine wengi kubadili jinsia zao kabisa.

Wiki iliyopita Cleopatra Kamburu alikabidhiwa hati yake mpya ya kusafiria na kitambulisho chake, kikimtambulisha kama mwanamke ambapo amesema alikuwa na matumaini ya muda mrefu kwamba siku moja ingewezekana kutambuliwa.

Lakini kupata hati na nyaraka hizo kulionekana kama hatua muhimu katika historia ya maisha yake, sawa na wakati wanawake waliporuhusiwa kupiga kura kwa mara ya kwanza. Alisema wakati hati yake ya kusafiria ilikuwa bado na herufi M (kwa maana ya kumtambua kama mwanaume), ilifika wakati ilimbidi avue nguo ili kuchunguzwa viungo vyake na kuthibitisha jinsia yake.

Anakumbuka siku moja tukio liliompomtokea: “Mtu mmoja aliniuliza, ‘Wewe ni mwanaume au mwanamke?’ lilikuwa jambo la aibu… huna haja ya kuangalia sehemu za siri za watu kujua wao kina nani?

“Tuna teknolojia ya kisasa ya ‘biometriska’ (teknolojia ya alama za vidole ama fingerprint au macho) kwenye mipaka. Nilimuuliza afisa wa uhamiaji, kama siwezi kutumia teknolojia hizo kujua mie ni nani. Kwa hiyo sikujua kwa nini nililazimika kuchunguzwa viungo vyangu vya uzazi,” amesema Cleopatra.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live