Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuo Kikuu cha Juba chapiga marufuku mikutano ya siasa

46a83030a0dc17a276f58f71f355e624 Chuo Kikuu cha Juba chapiga marufuku mikutano ya siasa

Tue, 10 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHUO Kikuu cha Juba kimepiga marufuku mikutano ya kisiasa ndani ya chuo hicho kwani inasumbua wahadhiri na kuonya kuwasimamisha kazi au kuwaachisha kazi ambao hawatatii.

Taarifa ya chuo hicho imesema hatua ya kuzuia mikutano hiyo imechukuliwa kutokana na kusababisha changamoto kwenye taaluma na katika mkutano wa maseneta ilibainika kuwa siasa ni moja ya vyanzo vya machafuko ambayo yanatishia utulivu wa kitaaluma wa vyuo vikuu.

"Seneti iilibaini matatizo ya kiwango cha juu yanayotokana na mikutano ya kisiasa, hivyo ili kukabiliana na hili mikutano ya kisiasa ikome mahali popote chuoni," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilionya kuwa mwanafunzi yeyote atakayekiuka agizo hilo atasimamishwa au kufukuzwa katika chuo kikuu hicho.

Oktoba Mosi mwaka huu utawala wa chuo hicho uliwasimamisha masomo baadhi ya wanafunzi kutokana na kushiriki maandamano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hiyo.

Wiki iliyopita wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Juba walijitokeza barabarani kupinga masuala kadhaa yaliyowekwa na uongozi wa chuo hicho ikiwamo kuzuia kuingia madarasani ambao hawajalipa ada ya masomo.

Chanzo: habarileo.co.tz