Chuo kikuu kimoja nchini Kenya kimeomba radhi kufuatia ya picha zilizosambaa mtandaoni za bango chuoni hapo linalosema kuwa ubakaji husababishwa na jinsi wanawake wanavyochagua kuvaa.
PUBLIC APOLOGY
— The Co-operative University of Kenya (CUK) (@CoopVarsityKE) November 26, 2021
For enquiries and clarifications:
Email: [email protected] / [email protected]
Website: https://t.co/1UIFxIRgzb pic.twitter.com/yAVIM0BZB6
Chuo Kikuu cha Ushirika cha Kenya kimekiri kwamba madai kwenye bango hilo - kwamba "mavazi yasiyofaa husababisha unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji" - yalikuwa ya uwongo.
Ilisema bango hilo ni"la kupotosha na la kusikitisha" linalohimiza kanuni za mavazi kwa wanafunzi lilikuwa limewekwa bila idhini yake na baraza la wanafunzi.
"Tunataka kuthibitisha dhamira yetu ya kuhakikisha kuwa aina zote za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji zinatokomezwa," taarifa ya chuo hicho ilisema: