Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chui ashambulia wanaume wawili kambi ya jeshi la wanahewa Afrika Kusini

Chui Ashambulia Wanaume Wawili Katika Kambi Ya Jeshi La Wanahewa Afrika Kusini.png Chui ashambulia wanaume wawili katika kambi ya jeshi la wanahewa Afrika Kusini

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Chui amewashambulia wanaume wawili katika kambi ya jeshi la wanahewa la Afrika Kusini ambalo linapakana na mbuga maarufu duniani ya Kruger National Park.

Mmoja wa waliovamiwa ambaye ni mwanajeshi, alikuwa ameenda kukimbia.

Mwingine, raia anayefanya kazi kwenye kituo hicho, alikutana na chui huyo akiwa anatembea, msemaji wa jeshi la wanahewa alisema.

Wawili hao walilazwa hospitalini wakiwa na mikwaruzo lakini hawakuwa na majeraha makubwa, Brig Jenerali Donavan Chetty aliambia BBC.

Mmoja ameruhusiwa kwenda nyumbani na mwingine anatarajiwa kuondoka siku ya Alhamisi.

Siku ya Jumatano, chui huyo alichukuliwa na kuhamishwa hadi kwenye hifadhi karibu kilomita 100 (maili 62) kutoka kambi ya jeshi la wanahewa la Hoedspruit, kufuatia mashambulizi ya wiki iliyopita.

Jenerali Chetty alisema kukutana na chui ni jambo la kawaida, lakini huwa sio hatari kwa wale wanaoishi na kufanya kazi karibu na mbuga hiyo.

Mbuga hiyo, ambayo ni kitovu cha utalii kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyamapori, imezungushiwa uzio.

Hata hivyo, Jenerali Chetty alisema ni vigumu kuzuia chui, ambao wanajulikana kuwa wepesi wa kuruka uzio.

Chui ni wanyama ambao huwa na shughuli nyingi nyakati za usiku hasa kutafuta mawindo mbalimbali, wakiwemo nyumbu, swala na samaki, tovuti ya Mbuga ya Kitaifa ya Kruger inasema.

Chanzo: Bbc