Chui mmoja amekamatwa na maafisa wa wanyamapori nchini Kenya baada ya kupotea na kwenda katika nyumba moja kusini-mashariki mwa Kenya.
Video ya askari wa wanyamapori wakiwa wamembeba chui huyo ambaye kichwa chake kilikuwa kimefunikwa, ilichapishwa na gazeti la Daily Nation:
KWS officers rescue a leopard that had entered a home in Voi, Taita Taveta County pic.twitter.com/in0Jg9wktu
— Nation Africa (@NationAfrica) December 16, 2021
Chui huyo anaaminika kupotea kutoka Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo hadi katika mji jirani wa Voi ambako alipatikana, vyombo vya habari nchini humo viliripoti.
Wakati wa kunaswa kwa chui huyo, wananchi waliizingira nyumba hiyo huku wakirekodi kwa simu zao.
Visa vya wanyama pori kupotea katika maeneo yaliyojengwa si jambo nadra nchini Kenya.
Shirika la Huduma ya Wanyamapori nchini Kenya hapo awali lilihimiza umma kuwa waangalifu na kuripoti wanyama wowote wanaozurura kupitia nambari isiyolipishwa.
Mnamo Julai, maafisa walimkamata simba ambaye alipatikana katika eneo la makazi karibu na jiji kuu la Nairobi.