Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Choo cha kinachopiga muziki kuwaburudisha wateja wanapojisaidia

Choo Cha Kinachopiga Muziki Choo cha kinachopiga muziki kuwaburudisha wateja wanapojisaidia

Fri, 29 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hii nayo kali! Wahudumu wa choo kimoja cha umma jijini Nairobi nchini Kenya wameamua kuboresha huduma kwa wateja wao kwa kuwawekea miziki katika vituo vyao vya huduma za kujisaidia.

Choo hicho ambacho kipo kando ya Barabara ya Tom Mboya, kimekuwa kikiwatumbuiza wateja wake kwa muziki mzuri huku wakiendelea na shughuli hiyo muhimi ya kibaolojia.

Wakati vipaza sauti vikiwa vimewekwa pasiko onekana, mhudumu huonekana ameketi kwenye kona, akicheza nyimbo kama 'DJ' kwa kuchanganya aina tofauti za muziki kulingana na wakati kama ni asubuhi, mchana ama usiku. Unaambiwa playlist ya nyimbo zao zimekuwa zikiwabamba vilivyo wateja wao.

"Hii ni burudani tunayowapa wateja wetu... na tumekuwa tukicheza muziki kwenye choo chetu kwa muda sasa..." mhudumu wa alisema wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari.

“Watu wanapenda muziki, na tunaamini kucheza aina tofauti za muziki kunaweza kusaidia kutoa msongo wa mawazo,” aliongeza mhudumu huyo, kulingana na nukuu katika wavuti huo.

Alipoulizwa kama wanacheza muziki kila wakati, Njeri anasema: "Hapana, si kila wakati. zaidi nyakati za jioni, siku za wiki hasa, tunapokuwa na wateja wengi."

Wateja wa choo hicho wanasema wanajisikia furaha kutumia huduma hiyo huku wakiburudika na kwamba huenda ndio chao pekee kinachocheza muziki, kuwaburudisha wateja, kuwarejesha hisia zao wanapoendelea na biashara zao kwenye sehemu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live