Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

China yatoa msaada wa dola 140,000 mafuriko Somalia

Maelfu Wakwama Katika Mafuriko Ya Somalia   UN China yatoa msaada wa dola 140,000 mafuriko Somalia

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ubalozi wa China nchini Somalia umeseema kuwa nchi yake imetoa msaada wa takriban dola 140,000 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Somalia walioathiriwa na mafuriko yanayoendelea kusababisha maafa na ambayo hadi hivi sasa yameshepelekea zaidi ya watu milioni 1 na laki 7 kuyahama makazi yao katika pembe mbalimbali za nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Akitangaza habari hiyo, Balozi Fei Shengchao wa China nchini Somalia amesema kuwa, fedha hizo zitatumika kutoa msaada wa kibinadamu kwa Wasomali walioathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo.

Amesema, wananchi wa China wameona jinsi wananchi wa Somalia wanavyoteseka kutokana na mafuriko makubwa, ambayo yameshapelekea zaidi ya watu 50 kupoteza maisha na wengine zaidi ya 700,000 kuyahama makazi yao kote nchini humo.

Eneo la Pembe ya Afrika limekumbwa na mafuriko makubwa kwa wiki kadhaa sasa baada ya nchi za eneo hilo kukumbwa na ukame wa miaka mingi. Mafuriko ya hivi sasa yameshasababisha zaidi ya watu mia moja kupoteza maisha na mamia kwa maelfu ya wengine kuhama makazi yao. Mafuriko eneo la Pembe ya Afrika yamesababisha maafa na wimbi la wakimbizi

Shirika la "Save the Children" limesema kwenye ripoti yake kwamba makumi ya watu wamefariki dunia mamia ya wengine wamelazimika kuyahama maeneo yao kutokana na mafuriko katika nchi zao. Taarifa ya shirika hilo imeongeza kuwa, hhali ya hewa ya El Nino imeongeza mvua katika eneo la Pembe ya Afrika na kuziathiri vibaya nchi mbalimbali hasa Somalia, Ethiopia na Kenya.

Eneo la Pembe ya Afrika ni moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi na mabadiliko hayo ya hali ya hewa, na matukio mengi ya kusikitisha yanaendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Tangu mwishoni mwa 2020, Somalia, pamoja na sehemu za Ethiopia na Kenya, zimeathirika kutokana na ukame mkubwa ambao ulikuwa haujawahi kushuhudiwa katika eneo hilo kwenye kipindi cha miaka 40.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live