Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

China yasisitiza kuiunga mkono Afrika kivitendo

Chinaaaaaaaa Afrikaaaa Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi amesisitiza nchi yake kuiunga mkono Afrika kivitendo kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana, Wang alizungumzia uhusiano kati ya nchi yake na Afrika akisema mawaziri wa mambo ya nje kila mwaka hutembelea Afrika, kitendo ambacho kinaonesha uungaji mkono imara kwa maendeleo na ufufukaji wa Afrika.

Wang alisema kwa miaka mingi, China imejenga zaidi ya kilometa 10,000 za reli, 100,000 za barabara, bandari zipatazo 100 pamoja na hospitali na shule zisizo na idadi barani Afrika. Alisisitiza kwamba hayo yamefanyika si mtego wa madeni bali ni alama za ushirikiano.

Alibainisha kuwa mwaka uliopita ulikuwa mzuri kwa ushirikiano wa China na Afrika, kwani pande mbili zilifanya kwa mafanikio Mkutano wa Nane wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

Katika mkutano huo, Xi Jinping alitangaza miradi tisa ya ushirikiano na Afrika, kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya Pamoja ya China na Afrika yenye hatima ya pamoja katika enzi mpya na kuongeza msukumo mpya katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika.

Aidha, alisema China itahimiza kwa nguvu moyo wa ushirikiano na urafiki kati yake na Afrika na kushirikiana na nchi za barani Afrika kwa kuzingatia kazi tatu.

Kazi hizo ni kuhimiza kwa nguvu ushirikiano katika mapambano dhidi ya janga la Covid-19; kuhimiza maboresho na kupandisha ngazi ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Afrika na kuhimiza wazo la Maendeleo ya Amani katika Pembe ya Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live