Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

China yaitupia lawama Marekani vikwazo vya uchumi Zimbabwe

Zimbabw Pic Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

China imeitupia lawama Marekani kwa kuiwekea Zimbambwe vikwazo vya kiuchumi kwa miaka 20 na kudai kuwa vikwazo hivyo vimeshusha kasi ya ukuaji wa uchumi katika taifa hilo la kusini wa Afrika.

Tamko hili la China lilitolewa mjini Beijing Oktoba 25, 2021 siku ambayo Zimbabwe ilikuwa ikiadhimisha siku ya kupinga vikwazo ilyoanzishwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC

Nae Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin amesema kuwa Marekani pamoja na mtaifa mengine ya Magharibi wanapaswa kuondoa vikwazo vyao haraka sana ili kuisaidia Zimbambwe kupambana na kasi ya maambukizi ya Corona.

"Vikwazo hivi vilivyowekwa na Marekani pamoja na mataifa mengine ya Magaharibi vimechangia kwa kiasi kikubwa kuua uchumi wa Zimbambwe, maisha ya watu nchini humo yamekuwa magumu sana" Amesema Wang.

Hata hivyo katika maadhimisho ya kupinga vikwazo hivyo kwa mwaka huu 2021, Mwandishi maalum kutoka umoja wa mataifa Alena Douhan alifika kwa ajili ya kufanya utafiti juu ya athari ziliojitokeza kufuatia vikwazo hivvyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live