Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

China yaahidi kuipa Tanzania ushirikiano mkubwa

C22fb9c88f90f11caf2c915e2df816f7.png China yaahidi kuipa Tanzania ushirikiano mkubwa

Tue, 1 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHINA imesema itafanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu ili kuiwezesha Tanzania kupiga kwa haraka hatua za kimaendeleo kwa faida ya pande zote mbili.

Hayo yamo katika barua ya pongezi iliyotumwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yikwenda kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi iliyowasilishwa kwake na Balozi wa China nchini, Wang Ke.

Akizungumza baada ya kukabidhi barua hiyo ya pongezi, Balozi Wang alisema China ina imani na Serikali ya Tanzania hususani baada ya Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba mwaka huu kwa utulivu na amani na kwamba imejipanga kuimarisha mahusiano ya kimkakati ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake, Profesa Kabudi alisema anazipokea kwa unyenyekevu salamu hizo za pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yina kuongeza kuwa katika mazungumzo yake na Balozi Wang Ke wameangazia zaidi masuala mbalimbali na ya kimkakati ya kutekeleza hususani yale yanayolenga katika hotuba ya Rais John Magufuli wakati akilifungua Bunge la 12 jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine, Profesa Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini, Anders Sjoberg na baadaye kukutana na kufanya mazun- gumzo na Balozi wa Finland nchini, Riitta Swan na kuzungumzia namna ya nchi hizo zitakavyoendelea kushirikiana katika nyanja za kiuchumi na kijamii ili kudu- misha urafiki, lakini pia kupiga hatua za kimaendeleo na kukuza uchumi.

Chanzo: habarileo.co.tz