Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chifu aliyekataa kusikia ushauri wa DP Gachagua akatwa nyeti

Chifu Aliyekataa Kusikia Ushauri Wa DP Gachagua Akatwa Nyeti.png Chifu aliyekataa kusikia ushauri wa DP Gachagua akatwa nyeti

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: Radio Jambo

Naibu Rais Rigathi Gachagua amehadithia kisa kimoja cha mwanaume aliyemwadhibu chifu wake baada ya kumshuku kuwa kuingilia nyumba yake.

Naibu Rais akiwa katika kaunti ya Tharaka Nithi aliwavunja mbavu machifu na viongozi waliohudhuria mkutano wa harakati za kukabili matumizi pombe haramu katika eneo hilo,alielezea kisa kimoja kilichofanyika alipokuwa Afisa wa wilaya mwaka wa 1995.

Kulingana na Naibu wa Rais mwanaume huyo alimwambia kuwa anasumbuliwa na chifu aliyekuwa ametwaa boma lake.

“1995, mtu akakuja akaniambia hii chifu yako ananisumbua na tutaonana hivi karibuni, amelalia kwangu. Anatumia crown ananitoa kwa boma yangu na tutaonana,” Rigathi alisema.

Naibu wa rais ambaye wakati huo alikuwa akihudumu kama mkuu wa taarafa (DO) aliwaonya machifu waliokuwa chini ya amri yake kuhusu onyo hilo kali kutoka kwa mwanaume huyo mwenye ghadhabu.

Kulingana na Gachagua chifu huyo hakusikia aliendelea kuramba asali kwa mzinga wa jirani lakini siku kumi tu baada ya onyo hilo, chifu huyo alikatwa nyeti na sehemu ya nyeti hiyo ikatundikwa kwenye mti katika soko la hapo karibu.

"Mimi si nabii, baada ya siku kumi tu baada ya kuwaonya machifu hawa, chifu alikatwa m*******de... ikawekwa kwa kamba ya kiatu na kuanikwa kwa soko.

Gachagua alikiri kuwa tangu tukio hilo kufanyika hakuna kesi ya chifu kuhusika katika mahusiano ya kimapenzi na wakazi wa eneo lake liliwahi kutokea.

"Baada ya miaka mingi nilipigia simu rafiki yangu akaniambia huko hakuna chifu anayekaribia bibi ya wenyewe."

Chanzo: Radio Jambo