Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chebukati: Cherera na wenzake walishinikiza uchaguzi urudiwe

Chebukati Cherera Chebukati: Cherera na wenzake walishinikiza uchaguzi urudiwe

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi (IEBC) Wafula Chebukati, amesema aliwazuia kuingia eneo la Bomas Makamishna wanne waliokana kutambua matokeo ya Urais kwa kulazimisha uchaguzi urudiwe.

Chebukati ameshikilia msimamo wake kuwa Makamishna hao wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa IEBC, Juliana Cherera walipata matokeo yote na walihusika katika shughuli zote za kuhakiki na kujumlisha Kura za Urais ambapo William Ruto alitangazwa kushinda.

Amefafanua pia kuhusu ongezeko la 0.01% ya Kura zilizolalamikiwa na Maafisa hao kuwa hazina ukweli na yeyote mwenye wasiwasi atembelee tovuti rasmi ya IEBC kupata taarifa sahihi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: