Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanjo ya covid-19 kutua hivi karibuni

277af03d0073e1e04ae9f2d6788b275d Chanjo ya covid-19 kutua hivi karibuni

Sun, 10 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI ya Sudan imesema ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo kwa ajili ya kupata chanjo ya ugonjwa wa covid- 19 kwa ajili ya wananchi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, mazungumzo hayo na kampuni ya Global Alliance for Vaccines (Gavi) yanakaribia kuzaa matunda, ambapo Sudan Kusini iliyopata Uhuru wake mwaka 2011 itapata mamilioni ya chanjo hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afya ya Kinga katika wizara hiyo, John Rumunu aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita kuwa, serikali inajiandaa kupokea shehena ya chanjo ya covid- 19 kutoka Gavi.

Mpango wa utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo duniani utasaidia kulipa gharama za mwanzo wakati huu yakifanya majaribio ya chanjo hiyo inayotarajiwa kuanza Januari mwaka huu.

“Serikali imeiomba Gavi kusaidia kulipia mzigo wa kwanza utakaofika siku chache zijazo,” alisema.

Rumunu alisema serikali imethibitisha kuwapo wagonjwa wa covid- 19 wapatao 5,210 kwa sasa na waliopona ni zaidi ya 3,131 na vifo hadi kufikia jana ni 63.

Taarifa ya idara hiyo iliyo ilisema ni haki ya Sudan Kusini kutoa chanjo kwa watu wake kama zinavyofanya nchi nyingine duniani.

Chanzo: habarileo.co.tz