Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanjo ya Sputnik V Huenda Ikaongeza Maambukizi ya HIV

Sputnik SA Sputnik V

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idara ya udhibiti wa bidhaa za afya nchini Afrika Kusini Sahpra, imezuia matumizi ya chanjo ya Urusi ya Sputnik V kwa hofu kwamba huenda ikaongeza hatari ya maambukizi ya virusi vya HIV miongoni mwa wanaume.

Uamuzi huo unatokana na tafiti mbili za awali ambazo zilipima usalama wa dawa aina ya adenovirusiliopo katika chanjo hiyo ya Urusi.

Taasisi ya Gamaleya , iliotengeneza chanjo ya Sputnik V, ilisema kwamba itatoa ushahidi kuonesha kwamba wasiwasi wa Sahpra sio wa kutiliwa maanani.

Taifa hilo lina idadi kubwa ya watu wanaoishi na maradhi ya HIV barani Afrika . Lina takriban watu milioni 7.8 wenye virusi hivyo katika idadi ya taifa hilo ya watu milioni 60, kulingana na UNAIDS.

Takriban asilimia 13.5 ya wanaume walio kati ya umri wa miaka 15 na 49 wameambukizwa.

Shirika la afya Duniani halijaidhinisha chanjo ya Sputnik V kwa matumizi ya dharura. Chanjo hiyo hatahivyo imekuwa ikitumika katika mataifa 45 ikiwemo Zimbabwe na Namibia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live