Umoja wa Mataifa umetangaza kuhusu mpango wa kuongezwa chanjo za malaria zitakazotolewa kote barani Afrika baada ya shehena ya kwanza ya dozi kuwasili Cameroon.
Tokea mwaka wa 2019, zaidi ya watoto milioni mbili wamepatiwa chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa malaria huko Ghana, Kenya na Malawi katika awamu ya majaribio, na kusababisha kupungua kwa ugonjwa huo hatarishi na kulazwa hospitalini.
Sasa mpango huo umejikita katika kutoa chanjo nyingi za kujikinga na ugonjwa wa malaria kukiwa tayari na dozi 331,200 za RTS,S - chanjo ya kwanza ya malaria iliyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Tayari baadhi ya chanjo hizo za malaria zimekwishawasili nchini Cameroon. Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na Muungano wa Pamoja wa Chanjo wa Gavi zimesema katika taarifa yao ya pamoja kuwa utoaji huu unaashiria kwamba nyongeza ya chanjo dhidi ya malaria katika maeneo hatarishi zaidi barani Afrika itaanza kutolewa hivi karibuni."
Unicef naMuungano wa Chanjo wa Gavi zimesema kuwa hatua hii ni ya kihistoria kuelekea ugawaji mkubwa wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo hatari zaidi unaowaathiri watoto wa Kiafrika".