Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanjo ya Ebola yawasili Uganda kwa majaribio

Chanjo Ya Ebola Yawasili Uganda Kwa Majaribio Chanjo ya Ebola yawasili Uganda kwa majaribio

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Waziri wa afya wa Uganda Alhamisi atapokea shehena ya chanjo ya Ebola ambayo itatumika katika majaribio ya kimatibabu.

Nchi hiyo imethibitisha kesi 142, na vifo 56, tangu ilipotangaza kuzuka kwa aina ya Ebola ya Sudan mnamo Septemba.

Katika ujumbe wa Twitter, msemaji wa wizara ya afya Emmanuel Ainebyoona alisema shehena hiyo itapokelewa kutoka kwa wawakilishi wa Shirika la Afya Duniani kwenye ghala karibu na mji mkuu, Kampala.

Waziri wa afya anatarajiwa kutangaza tarehe ya kuanza kwa majaribio, shirika la habari la AFP linaripoti.

Uganda haijasajili visa vipya vya ugonjwa wa Ebola kwa zaidi ya wiki tatu, hali inayoashiria kwamba mlipuko huo unaweza kuwa umedhibitiwa.

Chanzo: Bbc