Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama tawala nchini Cameroon chashinda viti vyote vya Bunge la Seneti

Camerooon Cha.jpeg Chama tawala nchini Cameroon chashinda viti vyote vya Bunge la Seneti

Sun, 26 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama tawala cha Rais Paul Biya, ambaye anatawala nchini Cameroon bila kugawana madaraka kwa zaidi ya miaka 40, kimeshinda viti vyote 70 katika Bunge la Seneti katika uchaguzi uliyofanyika Machi 12.

Tangazo hilo limetolewa na Baraza la Katiba la Cameroon ambalo limesema, wapinzani hawakufanikiwa kupata hata kiti kimoja katika uchaguzi wa mara hii.

Rais Paul Biya, mwenye umri wa miaka 90 atateua ndani ya siku 10 zijazo maseneta zaidi 30.

Chama tawala cha RDPC kimeimarisha utawala wake wote katika Bunge la Seneti kwani upinzani ulikuwa na viti saba katika Bunge la Seneti linalomaliza muda wake.

Chama tawala nchini Cameroon kimeshinda viti vyote katika kila moja ya mikoa, kulingana na matokeo yaliyosomwa na Clément Atangana, Mwenyekiti wa Baraza la Katiba, wakati wa hafla iliyoruswa hewani moja kwa moja kwenye televisheni ya serikali, CRTV.

RDPC kilikuwa chama pekee kuwa na orodha katika mikoa yote kumi. Kinadhibiti manispaa 316 kati ya 360 nchini Cameroon. Katika Bunge la Kitaifa, Chama cha Rais Paul Biya na washirika wake pia wana idadi kubwa ya wabunge 164 kati ya 180, waliochaguliwa mnamo mwezi Februari 2020.

Paul Biya anaongoza Cameroon tangu 1982 kwa mkono wa chuma, ambaye anashtumiwa mara kwa mara na Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa kukandamiza upinzani na waasi wanaotaka mikoa yao kujittawala katika mikoa miwili ya Magharibi inayozungumza Kiingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live