Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama tawala Kenya chaungana na upinzani

Kenyatta Pic Dataeded Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya

Sun, 27 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama tawala Kenya kimeungana na upinzani kuelekea uchaguzi mkuu

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana Jumamosi amesema chama chake kimeungana na muungano wa upinzani kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti kwa kile alichodai jitihada ya kusafisha siasa za kifisadi.

Tangazo hilo linatolewa wakati makamo wake ambae pia anataka kuwania kiti cha urais, William Ruto, akifukuzwa kutoka katika chama tawala cha Jubilee. Kenyatta alisikika akihoji ukosoaji uliosema

"Hakuna kokote duniani ambapo serikali inaungana na upinzani" na kuongeza kwamba chama chake kimeungana na Azimio la Umoja, muungano ambao unaongozwa na mwanasiasa mkongwe Raila Odinga.Rais Kenyatta amesema Kenya itakuwa mfano.

Wamekomaa kisiasa kwa kiasi cha kutosha, kwa kuweza kutenganisha siasa na matakwa ya watu. Awali Ruto ndio alitazamwa kama mrithi wa Kenyatta katika chama hicho tawala, lakini baadae akajikuta akitengwa kufuatia hatua ya waliokuwa mahasimu wakubwa Kenyatta na Odinga kutangaza maridhiano 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live