Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama cha Upinzani Guinea chaunga mkono "Jeshi la Mapinduzi"

Guinea Chama cha upinzani Guinea, chaunga mkono jeshi la mapinduzi

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiogozi wa upinzani nchini Guinea, Cellou Diallo amesema yupo tayari kufanya kazi na jeshi lililofanya mapinduzi nchini humo tarehe 05 septemba mwaka 2021.

Kiongozi huyo, anaungana na maelfu ya wananchi wa nchini humo waliofurahia kitendo hicho cha wanajeshi kumpindua Rais Alpha Conde kwa tuhuma za uongozi mbovu na kukithiri kwa vitendo vya rushwa.

Diallo amenukuliwa akisema kuwa, Chama chake cha National Committee for Rally and Development CNRD, kitatoa ushirikiano kwa Jeshi hilo ili kujenga Serikali yenye kuzingatia uhuru na usawa kwa wote.

"Chama chetu cha CNRD, kipo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la mapinduzi ili kujenga Serikali yenye usawa, hii ndio nafasi yetu kuwaonesha wananchi wa Guinea ndani na nnje ya nchi, walioambana katika kuondoa mfumo huu wa udikteta" amesema kiongozi huyo wa upinzani.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wanaohofia Jeshi hilo linaweza likachelewa kurudisha Serikali ya kiraia licha ya kuwa tayari wameshaweka bayana mpango wa kufanya mchakato wa kurejesha Serikali kwa wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live