Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama cha UDA kinachohusiana na DP Ruto kufungua Ofisi Marekani

F38b833c7bdba62a Chama cha UDA kinachohusiana na DP Ruto kufungua Ofisi Marekani

Mon, 14 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Sherehe hiyo imeratibiwa kufanyika Ijumaa, Juni 18, mwendo wa saa kumi na mbili jioniHafla hiyo itaongozwa na Seneta Irungu Kang'ata Ofisi ya chama hicho itafunguliwa mjini Seattle katika jimbo la Washington

Chama cha United Democratic Party (UDA), kinachohusiana na Naibu Rais William Ruto, kinatazamiwa kufungua tawi lake nchini Marekani.

Sherehe hiyo imeratibiwa kufanyika Ijumaa, Juni 18, mwendo wa saa kumi na mbili jioni na itaongozwa na Seneta wa Murang'a Irungu Kang'ata.

Kulingana na ujumbe uliotolewa na seneta huyo kwenye ukurasa wake wa Facebook, mwenyekiti mwandamizi wa chama hicho nchini Marekani Kiarie Prestige ndiye atakuwa mwenyeji wa hafla hiyo.

Kang'ata pia alifichua kuwa ofisi ya chama hicho itafunguliwa mjini Seattle katika jimbo la Washington.

"Kwa heshima na nafurahia kuwa Mgeni Muheshimwa katika uzinduzi wa ofisi ya UDA mjini Seattle USA Washington, mtaa nambari 1648 310th, Federal Way Washington 98003 mnamo Juni, 18 2021 saa kumi na mbili jioni. Wote wanakaribishwa," alisema Kang'ata.

UDA kilibadilisha jina lake kutoka Party of Development and Reforms (PDR) ambacho ni chama tanzu cha mrengowa Jubilee mnamo Disemba 2020.

Kisha ilibadilisha kauli mbiu kutoka kwa Mabadiliko na Ustawi to Kazi ni Kazi na kuweka nembo ya wilibaro.

Kisha Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen alithibitisha kuwa mrengo wa chama cha Jubilee, Tanga Tanga utahamia chama cha UDA hivi karibuni.

Murkomen ambaye ni mshirika wa karibu wa Ruto alisema uhusiano kati ya kundi la Tangatanga na Kieleweke ulidorora na hivyo waliamua kutengana na kubuni chama kipya.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke