Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama cha Majaji Tunisia chasimamisha shughuli zote za Mahakama

Kais Said Kais Saed, Rais wa Tunisia

Wed, 9 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha majaji nchini Tunisia kimetoa wito wa kusitishwa shughuli zote katika mahakama za nchi hiyo kuanzia kesho Februari 9 na 10 ili kupinga hatua iliyochukuliwa na Rais wa nchi hiyo Kais Saed ya kulivunja baraza la mahakama ya juu kabisa.

Chama hicho kimetoa wito huo kupitia ujumbe wake kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na kusitisha maandamano ya baraza la mahakama ya juu yaliyopangwa kufanyika siku ya alhamisi.

Aidha mabalozi wa Tunisia katika nchi tajiri duniani kutoka kenye kundi la G7 wametoa mitazamo yao kuhusu hatua hiyo ya Rais Saed huku wengi wakishuku maamuzi hayo kuwa hayana nia njema.

Uamuzi wa rais huyo umekuja miezi kadhaa baada ya kuwafuta kazi mawaziri wake wote na kutwaa mamlaka yote ya kuingoza Tunisia kwa amri moja ya rais.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live