Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama cha ANC cha Afrika kusini kinataabika kupata asilimia 50 ya kura

Chama Cha ANC Cha Afrika Kusini Kinataabika Kupata Asilimia 50 Ya Kura Chama cha ANC cha Afrika kusini kinataabika kupata asilimia 50 ya kura

Fri, 31 May 2024 Chanzo: Voa

Kama ANC kitashindwa itakuwa ni mara ya kwanza kupoteza viti vyake vingi bungeni tangu kumalizika ubaguzi wa rangi 1994. Chama cha Afrika Kusini cha African National Congress, ambacho kilipata madaraka chini ya Rais Nelson Mandela, kimepata chini ya asilimia 50 ya kura katika matokeo ya awali ya uchaguzi.

Kama ANC kitashindwa itakuwa ni mara ya kwanza kupoteza viti vyake vingi bungeni tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

Takriban asilimia 27 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa Jumatano zimehesabiwa kufikia Alhamisi. Tume huru ya uchaguzi imesema kura za mwisho zitawasilishwa siku ya Jumapili. ANC ina asilimia 43 ya kura zilizotokana na matokeo kutoka kwa vituo 6,000 kati ya 23,000 vya kupigia kura katika majimbo tisa ya Afrika Kusini.

Kama ANC hakitapata wingi wa viti, kitahitaji kuungwa mkono na vyama vingine ili kumchagua tena Rais Cyril Ramaphosa kwa muhula wa pili.

Chanzo: Voa