Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amemsamehe waziri aliyekuwa na ushawishi mkubwa nchini humo, Uladi Mussa ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kutumia vibaya madaraka yake.
Waziri wa Usalama wa Ndani ya Nchi, Ken Zikhale Ng’oma akizungumzia suala hilo amesema kuachiliwa kwake ni kitendo cha huruma katika msimu wa Sikukuu ya Pasaka.
Kiongozi huyo wa zamani aliachiliwa huru pamoja na wafungwa wengine 199 waliofanya makosa madogo ambao walionyesha tabia nzuri wakati walipokuwa gerezani.
Uladi ameendelea kuwa na ushawishi katika siasa za nchini humo baada ya kuhudumu kama waziri chini ya marais wanne kati ya mwaka 1994 na 2019.