Kiongozi wa taifa aliwaonya Wakenya dhidi ya siasa na badala yake kuwachagua viongozi ambao wako tayari kufanya mabadilikoRais pia aliwataka Wakenya kuwachagua viongozi walio tayari kuchukua maamuzi ya kijasiri dhidi ya wanasiasa wanaopenda umaarufu
Uhuru alizitaja miradi ambazo anatumainia kukamilisha kabla ya kuondoka madarakani Agosti 2021Rais Uhuru Kenyatta amewaomba Wakenya kuchagua uongozi badala ya siasa katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Katika hotuba yake ya mwisho ya Mwaka Mpya siku ya Ijumaa,Disemba 31, kiongozi wa taifa aliwaonya Wakenya dhidi ya siasa na badala yake kuwachagua viongozi ambao wako tayari kufanya mabadiliko.
“Uongozi ni maono; siasa ni vyeo. Uongozi unahusu kizazi kijacho; siasa ni uchaguzi ujao. Na kuhangaikia kwetu siasa kumepunguza kasi ya utambuzi wa uwezo wetu kama watu,” alisema Kenyatta.
Rais pia aliwataka Wakenya kuwachagua viongozi walio tayari kuchukua maamuzi ya kijasiri dhidi ya wanasiasa wanaopenda umaarufu.
"Kenya lazima ichague njia ya ujasiri juu ya njia maarufu. Ni lazima tuchague wachache wakosoaji walio na ujasiri kuliko walio wengi wasio na maana. Na kuna mifano kote ulimwenguni ambapo wajasiri walishinda maarufu. "alisema.
"Na mwanasiasa huchukua njia maarufu ambayo inampendeza kila mtu, lakini haiwapeleki popote. Ikiwa tunataka kuwa 'taifa la kuzuka', lazima tufuate mashujaa," aliongeza rais.
Miezi saba aondoke madarakaniZikiwa zimesalia miezi saba muhula wake kukamilika, utawala wa Jubilee sasa utakuwa kwenye pilikapilika ya kufanikisha miradi ya maendeleo katika kipindi hicho.
Rais alizitaja miradi ambazo anatumainia kukamilisha kabla ya kuondoka madarakani Agosti 2021.
Katika sekta ya afya, kiongozi wa taifa alisema ana matumaini ya kufanikisha mradi wa kutoa afya bora yenye bei nafuu kwa Wakenya wote mwaka 2022.
Kuhusu elimu, Rais anapania kujenga madarasa 10,000 mapya ili kufanikisa mtaala mpya wa elimu wa CBC.
Kwenye uchukuzi, Uhuru anapania kuwacha rekodi ya maendeleo kwa kuzindua barabara ya kisasa ya Nairobi Expressway mnamo April ili kupunguza msongamano wa magari.
Pia kufungua barabara ya Kisumu Mamboleo, Eldoret Bypass, na barabara ya Kenol-Marua.
Japo ahadi yake ya kupunguza gharama ya umeme bado haijaanza kutekelezwa, rais ameahidi kutekeleza ahadi hiyo kuanzia Machi 2022.