Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadi: Zoezi la kuhesabu kura mchakto katiba mpya laanza

Chad Yaanza Kufanya Kampeni Kupigia Kura Katiba Mpya Chadi: Zoezi la kuhesabu kura mchakto katiba mpya laanza

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Chad baada ya wananchi kushiriki kura ya maoni juu ya katiba mpya iliyoahidiwa na utawala wa kijeshi, japo imepingwa na wanasiasa wa upinzani Nchini humo

Ishara zote zinaonyesha kuwa Katiba Mpya itaidhinishwa na kufungua njia kuelekea kufanyika kwa uchaguzi na hivyo kurudi kwa utawala wa kiraia

Hata hivyo, idadi kubwa ya wapinzani na mashirika ya kiraia katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati yametoa wito kwa wananchi kususia kura hiyo iliyopigwa Jumapili Desemba 17.2023

Upinzani umeeleza kuwa kura hiyo imeandaliwa kama mbinu ya kumfungulia njia Rais wa sasa wa mpito Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno kuendelea kusalia madarakani na kuendeleza siasa za 'urithi' zilizoanzishwa na Marehemu Baba yake miaka 33 iliyopita kufuatia mapinduzi ya kijeshi

Kambi ya 'ndio' inaonekana kuwa na uhakika wa ushindi baada ya kampeni ilivyofadhiliwa na utawala wa kijeshi dhidi ya upinzani uliogawanyika na ambao wanachama wake wamekamatwa na kukabiliwa na vitisho vya mara kwa mara

Chanzo: www.tanzaniaweb.live