Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chad yataifisha mali zote za Exxon Mobil

EXXON MOBIL.png Chad yataifisha mali zote za Exxon Mobil

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI ya Chad imetaifisha mali zote kutoka kwa kampuni kubwa ya kimataifa ya mafuta ya Exxon Mobil, ikiwa ni pamoja na vibali vyake utafutaji mafuta na vya hydrocarbon.

″Waziri wa fedha na bajeti lazima ahakikishe kuwa agizo hilo linatekelezwa kuanzia tarehe ya kuchapishwa kwake,” alisema Katibu Mkuu wa serikali Haliki Choua Mahamat kwenye taarifa yakw kwa vyombo vya habari vya serikali.

Kutaifishwa kwa kampuni binafsi kunamaanisha kuwa mali zote sasa zinamilikiwa na serikali. Ingawa hii iliwahi kutokea katika miaka ya 1960 na 1970, haijafanyika hivi karibuni na hailingani na mifumo ya kawaida ya kisheria katika sekta hiyo, wataalamu wa nishati wamesema.

Chad ilianza kuzalisha mafuta mwaka 2003 na Exxon imekuwa ikifanya kazi nchini humo kwa miongo kadhaa. Ilikuwa inaendesha mradi wa mafuta wa Doba nchini Chad.

Hatua hiyo inaweza kuwaogopesha wawekezaji kutoka Afŕika Maghaŕibi wakati wa kuongezeka kwa mahitaji ya nishati duniani na kupungua kwa uwekezaji wa kigeni katika kanda, alisema Olufola Wusu, mshiŕika na mkuu wa dawati la mafuta na gesi katika taasisi ya Megathos Law Practice yenye makao yake makuu nchini Nigeŕia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live