Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chad kufanya uchaguzi wa kwanza baada ya miaka 3

Chad Kufanya Uchaguzi Wa Rais Baada Ya Miaka 3 Chad kufanya uchaguzi wa kwanza baada ya miaka 3

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Tume ya uchaguzi ya Chad, imesema duru ya kwanza ya uchaguzi wa Rais itafanyika Mei 6, 2024 ukiwa wa kwanza tangu kumalizika kwa utawala wa kiraia.

Kura hizo za maoni zitaashiria mwisho wa kipindi kirefu cha mpito cha kijeshi ambacho kilianza mwaka 2021, baada ya kifo cha kiongozi wa muda mrefu, Idriss Deby Itno.

Kulingana na kalenda ya uchaguzi iliyochapishwa jana Jumanne, Februari 27, 2024 duru ya pili ya upigaji kura itaandaliwa Juni na matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa Julai, mwaka huu.

Rais wa tume ya uchaguzi, Ahmet Bartchiret amesema ilikuwa ni lazima uchaguzi ufanyike kabla ya Oktoba 10, tarehe ambayo kipindi cha mpito cha kijeshi kinastahili kumalizika.

Mahamat Idriss Deby, ameongoza nchi kwa karibu miaka mitatu sasa, licha ya ahadi ya awali ya kuondoka baada ya kipindi cha mpito cha miezi 18.

Kipindi cha mpito kiliongezwa baadaye kwa miaka miwili, hivyo kurefusha kukaa kwake madarakani.

Chanzo: Bbc