Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chad: Rasimu katiba mpya yapitishwa kwa asilimia 86

Chad Yaanza Kufanya Kampeni Kupigia Kura Katiba Mpya Chad: Rasimu katiba mpya yapitishwa kwa asilimia 86

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Uchaguzi nchini Chad imetangaza kwamba rasimu ya Katiba Mpya iliyopigiwa kura wiki moja iliyopita imeidhinishwa kwa asilimia 86

Hata hivyo, matokeo hayo yamepingwa mara moja na viongozi kadhaa wa upinzani Nchini humo

Tangazo la Tume hiyo limesema idadi ya wapiga kura waliojitokeza ilikuwa asilimia 63.75 na kwamba licha ya hitilafu ndogo zilizoshuhudiwa wakati wa zoezi la kupiga kura, lakini kura hiyo ya maoni ilifanyika vizuri

Matokeo rasmi ya kura hiyo yatasubiri kuidhinishwa na Mahakama ya Juu ya Taifa hilo mnamo Desemba 28 mwaka huu

Watawala wa Kijeshi wa Chad wameipigia upatu rasimu ya katiba iliyopitishwa kuwa hatua muhimu kuelekea kuirejesha Chad chini ya utawala wa kiraia

Lakini upinzani na wanaharakati wengine wameyapinga madai hayo na wametoa wito kwa wafuasi wao kuisusia kura hiyo ya maoni iliyofanyika Disemba 17 mwaka huu

Upinzani pia umeyapinga matokeo ya kura hiyo na umesema takwimu zilizotolewa juu ya idadi ya wapiga kura ni za uongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live