Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cameroon yatoa chanjo ya kwanza ya malaria duniani

Cameroon Yatoa Chanjo Ya Kwanza Ya Malaria Duniani Cameroon yatoa chanjo ya kwanza ya malaria duniani

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Cameroon imezindua mpango wa kwanza duniani wa chanjo dhidi ya malaria, katika mapambano ya kimataifa yanayotarajiwa kuokoa maelfu ya maisha ya watoto kote barani Afrika.

Chanjo ya RTS,S iliyoidhinishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), iliyotengenezwa na mtengenezaji wa dawa wa Uingereza GSK, inalenga watoto wachanga katika wilaya 42 zilizoathiriwa zaidi nchini Cameroon.

Nchi hiyo ya Afrika ya kati itakuwa nchi ya kwanza kutoa dozi kupitia mpango wa kawaida wa chanjo, kufuatia kampeni za majaribio zilizofanikiwa nchini Kenya, Ghana na Malawi.

Utoaji huo, unaotarajiwa kuanza Jumatatu, ulielezwa na maafisa wa afya kama hatua muhimu katika juhudi za miongo kadhaa za kukabiliana na ugonjwa wa malaria barani humo.

Nchi nyingine 20 zinalenga kuzindua mpango huo mwaka huu, kulingana na muungano wa kimataifa wa chanjo Gavi.

Chanjo ya dozi nne inafanya kazi kwa takriban 30% tu na kinga huanza kufifia baada ya miezi kadhaa.

GSK ilisema inaweza kutoa takriban dozi milioni 15 tu kwa mwaka.

Chanzo: Bbc