Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cameroon: Serikali yapiga marufuku kuuliza alipo Rais Biya

Paul Biya Cameroon: Serikali yapiga marufuku kuuliza alipo Rais Biya

Fri, 11 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Cameroon imepiga marufuku mijadala ya Wananchi kuhusu hali ya kiafya na mahali alipo Rais Paul Biya (91) ikidaiwa mijadala hiyo inahatarisha Usalama wa Nchi

Hali hiyo inafuatia kutoonekana hadharani kwa Kiongozi huyo ambaye mara ya mwisho alihudhuria Mkutano wa Ushirika kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing Septemba 8, 2024

Magavana wameagizwa kuunda vikosi vya kufuatilia na kurekodi vipindi na mijadala inayohusu Afya ya Biya inayofanyika kwa siri au hadharani na kuzitaarifu mamlaka

Ikumbukwe, Biya ndiye Rais mzee zaidi duniani ambaye bado yuko madarakani akiwa ni Rais wa awamu ya pili na aliyeitawala Cameroon tangu Novemba 6, 1982.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live