Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cameroon: Hatutamruhusu balozi wa Ufaransa kuja nchini kupigia debe ushoga

Cameroon Flag Cameroon: Hatutamruhusu balozi wa Ufaransa kuja nchini kupigia debe ushoga

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Cameroon imesema haitamruhusu kuingia nchini humo balozi wa Ufaransa wa kutetea na kushajiisha vitendo vya ushoga, usagaji na watu kubadili jinsia zao (LGBT).

Balozi huyo wa Ufaransa, Jean-Marc Berthon ameratibiwa kwenda Cameroon kushiriki kongamano la kushajiisha vitendo hivyo vya ufuska, linalotazamiwa kufanyika baina ya Juni 27 na Julai Mosi katika mji mkuu Yaounde.

Kongamano hilo la kuwashawishi vijana wajihusishe na ubaradhuli linaandaliwa na taasisi moja ya Kifaransa. Hata hivyo maafisa wa serikali ya Cameroon wamesisitiza kuwa hawatamruhusu afisa huyo wa Ufaransa nchini kwao kwenda kupigia debe uchafu huo.

Aghalabu ya nchi za Afrika zinapinga vitendo vya ushoga na usagaji na watu kubadilisha jinsia zao. Baadhi ya nchi hizo zina sheria kali za kukabiliana na mienendo hiyo inayokwenda kinyume na maumbile ya mwanadamu.

Hivi karibuni, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, alikataa wito wa nchi za Magharibi wa kufuta sheria dhidi ya ushoga iliyopasishwa na Bunge la nchi hiyo na kuidhinishwa na yeye mwenyewe. Wananchi wa Senegal wakiandamana kupinga ubaradhuli nchini humo

Sheria hiyo iliyotiwa saini na Rais Museveni inatoa adhabu kali kwa wahalifu wanaopatikakana na hatia ya kujihusisha na vitendo vichafu cha ushoga.

Aidha Bunge la Ghana linatazamiwa kupasisha muswada dhidi ya mahusiano ya watu wenye jinsia moja ambao unaainisha hadi kifungo cha miaka 10 jela kwa wale watakaojihusiha na uovu huo au kuushajiisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live