MAOFISA nchini Ghana wamesema kuwa ndege ambazo zinawasafirisha raia wa kigeni ambao hawajachanjwa ndani ya taifa hilo zitapigwa faini ya dola $3,500 (Tsh milioni 8) kwa kila msafiri.
Makamouni ya ndege pia yanapaswa kuhakikisha kwamba watu wanajaza fomu zinazoelezea hali zao za kiafya. Muongozo mpya ambao unaanza kutekelezwa Jumanne unalenga kuzuwia kusambaa kwa Covid-19 aina ya Omicron.
Faini hiyo inalenga kuimarisha marufuku kwa wageni wa kigeni ambao hawajapokea chanjo ya virusi vua corona ambao wanazuiwa kuingia nchini Ghana, marufuku inayoanza kutekelezwa leo Jumatatu.
Raia wa Ghana pamoja na wakazi wanaoishi nje ya nchi hiyo hawatahusishwa na marufuku hiyo kwa wiki mbili zijazo, lakini watapaswa kupata chanjo watakapowasili kwenye uwanja wa ndege. Maafisa wanasema kuwa wanahfia juu ya ongezeko la maambukizi katika kipindi cha msimu wa sherehe.
Wasafiri wote wanatakiwa kuonyesha matokeo hasi ya kipimo cha PCR kinachofanyika katika kipindi cha saa 72 za kuondoka na pia watapimwa kwenye uwanja wa ndege mara wanapowasili. Ghana imewachaja chini ya 10% ya watu wake milioni 30.