Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

COVID: RwandaAir yasitisha safari za Uganda

Rwandair 1 984x554 1 660x400.jpeg COVID: RwandaAir yasitisha safari za Uganda

Sat, 12 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir imetangaza kuwa imesitisha kwa muda safari zake za ndege za kwenda na kutoka kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Uganda wa Entebbe mara moja.

“Kutokana na kuongezeka kwa visa vya Covid-19 nchini Uganda, RwandAir inatangaza kusitishwa kwa safari zake za ndege za kuelekea na kutoka Entebbe kuanzia tarehe 10 Juni 2021, hadi tangazo lingine litakapotolewa, RwandAir inaomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na hatua hiyo.” Taarifa ya shirika hilo la ndege ya Rwanda

Shirika hilo lilisema kuwa wateja waliothiriwa ‘’wanaweza kupanga upya safari na kusafiri baadaye, pale safari hizo zitakaporejeshwa tena au waombe kurejeshewa pesa zao za nauli.”

Chanzo: millardayo.com