Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

COVID-19: Wagonjwa 14 zaidi wapoteza maisha yao huku visa 394 vikirekodiwa

72e8e977b2c7ba00.jpeg COVID-19: Wagonjwa 14 zaidi wapoteza maisha yao huku visa 394 vikirekodiwa

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Jumla ya waliofariki dunia imefika 2,258 baada ya wagonjwa wengine 14 kuangamizwa katika takwimu za hivi punde

- Wakati huo huo Wizara ya Afya ilionesha kuwa wagonjwa 2,217 wamepta nafuu katika saa 24 zilizopita

- Jumla ya Wakenya 325,592 wamepewa chanjo, huku kaunti za Nairobi, Nakuru, Uasin Gishu, Kisumu, na Kiambu zikiandikisha idadi kubwa zaidi ya walichanjwa

Jumla ya watu 394 wamepimwa na kudhibitishwa kuambukizwa Covid-19 kutokana na sampuli 2,923 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa jumla ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya Covid-19 imefika 139,842 huku idadi ya sampuli zilizopimwa tangu mwezi Machi kugonga 1,523,313.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ilionyesha kuwa idadi ya wagonjwa 2,217 wamepona katika saa ishirini na nne ziliyopita. Jumla ya wagonjwa waliopata nafuu imefika 96,578.

Kati ya visa vilivyotangazwa, jumla ya Wakenya waliorekodiwa kupata maambukizi ni 374 wakati raia wa kigeni nao wakiwa 20 ni wageni. Wagonjwa 209 ni wanaume na 185 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ni mtoto wa miezi minane naye mkongwe zaidi ana miaka 95.

Hata hivyo wakato uo huo watu vifo 14 wameripotiwa kupoteza maisha yao kutokana na makali ya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,576 kwa sasa wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya nchini kote, huku wagonjwa 6,182 nao wakihudumiwa wakiwa manyumbani mwao.

Wagonjwa 205 wako katika Kitengo cha Huduma Mahututi (ICU), 46 kati yao wakiongezewa oksijeni.

Nairobi inaendelea kuongoza kwa visa 246, ikifuatiwa kwa mbali na Kiambu (29), Machakos (23), Uasin Gishu (22) na Kitui (20).

Jumla ya Wakenya 325,592 wamepewa chanjo, huku kaunti za Nairobi, Nakuru, Uasin Gishu, Kisumu, na Kiambu zikiandikisha idadi kubwa zaidi ya waliochanjwa.

Nairobi, 108,180, Nakuru, 23,511, Uasin Gishu 18,516, Kisumu, 13,644 na Kiambu 13,623.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke