Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

COVID-19: Sudan Kusini yaharibu chanjo 60,000 za aina ya AstraZenica

46ca529c6499dc84 COVID-19: Sudan Kusini yaharibu chanjo 60,000 za aina ya AstraZenica

Wed, 21 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Serikali ya Sudan Kusini imeharibu chanjo 60,000 za virusi vya ugonjwa wa corona ikidai kwamba ziliwasili nchini humo kama muda wa kuharibika ulikuwa umefika.

Kwa mujibu wa taarifa za BBC, Chanjo hizo zilikuwa zimetolewa kama msaada kutoka kwa kampuni ya Afrika ya mawasiliano MTN na Muungano wa Afrika wiki kadhaa zilizopita.

Wataalamu kutoka mataifa mbali mbali wamekashifu hatua ya Sudan Kusini kuharibu chanjo hizo kabla ya kufuata maagizo inavyostahili.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Muungano wa Afrika CDC John Nkegasong amesema serikali ya Sudan Kusini ilikuwa na muda wa kutosha kutumia chanjo hizo kabla hazijaharibika.

Malawi ni nchi nyingine ambayo imekuwa ikipinga vikali matumizi ya chanjo hizo na tayari ilikuwa imepanga kuziharibu.

Haya yanajiri wakati ambapo nchi zingine Barani Afrika zikihangaika kupata chanjo za kutosha kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya COVID-19.

Kama ilivyoripotiwa awali, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alipokea chanjo ya ugonjwa wa corona wiki iliyopita.

Hapa Kenya viongozi kadhaa akiwemo Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Wake William Ruto, kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi tayari wamepokea chanjo hiyo.

Kufikia Alhamisi Aprili 15, watu 28,234 walikuwa wamepokea chanjo na ya AstraZeneca na kufanya idadi kamili kugonga 651,650.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke