Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CIA wabainika kuhusika tukio la kumkamata Mandela

MANDELA JELA CIA wabainika kuhusika tukio la kumkamata Mandela

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchunguzi umebaini kuwa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA, lilihusika katika kukamatwa kwa Nelson Mandela, aliyekuwa kiongozi wa mapambano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Richard Stengel, ripota wa zamani wa jarida la Time, aliandika katika makala yake ya jana Jumatatu kwamba: Ripoti mpya ya uchunguzi inaonyesha kwamba Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) huenda lilihusika katika kukamatwa kwa Nelson Mandela, kiongozi wa upinzani dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Maelezo mapya kuhusu nafasi ya CIA katika kukamatwa kwa Mandela yalifichuka wakati Richard Stengel, ambaye alishiriki kutayarisha wasifu wa Mandela, alipokuwa akipitia mahojiano yaliyorekodiwa hapo awali na kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini.

Katika mahojiano ya 1993, Mandela alimwambia Stengel kwamba kulikuwa na uvumi kwamba CIA iliwatonya polisi wa Afrika Kusini kuhusu mahali alipokuwa amejificha.

Habari hii inatiwa nguvu na makala nyingine iliyochapishwa mwaka 1986 katika jarida la Afrika Kusini. Jarida la "Johannesburg Star" mwaka huo lilimnukuu afisa wa polisi aliyestaafu na kuandika kwamba polisi wa Afrika Kusini wamepata taarifa muhimu katika kesi hii kutoka kwa "ajenti wa CIA katika eneo hilo".

Aidha, takriban miaka sita iliyopita, Donald Rickard, jasusi wa zamani wa CIA, alikiri kwamba utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ulishirikiana na shirika la CIA kumkamata Nelson Mandela, kiongozi wa harakati za ukombozi wa Afrika Kusini.

Baada ya kuongoza harakati ya kupinga ubaguzi wa rangi, Mandela alikuwa mzalendo mweusi wa kwanza kushika wadhifa wa urais wa Afrika Kusini kuanzia mwaka 1994 hadi 1999.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live