Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHAD: Ndani ya miezi mitatu raia 500 wameuawa kwa mapigano

Chad 500 Raia Ndani ya miezi mitatu raia 500 wameuawa kwa mapigano

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, raia zaidi ya 500 wameuawa nchini Mali katika mapigano kati ya jeshi na wanamgambo yaliyojiri kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Mali imeeleza kuwa, katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi, yamesajiliwa pia matukio ya zaidi ya 320 ya ukiukaji haki za binadamu yaliyofanywa na jeshi la serikali, wakati idadi ya matukio hayo katika miezi mitatu ya kabla yake ilikuwa ni 32 tu.

Kwa mujibu wa UN takwimu hizo zinamaanisha kuwa katika muda wa miezi mitatu, maafa ya roho za watu yameongezeka kwa asilimia 320 kulinganisha na miezi mitatu ya kabla ya hapo na kuonyesha pia kwamba utawala wa kijeshi wa Mali umeshindwa kudhibiti ukiukaji wa haki za binadamu au kukabiliana na hatua za ukatili na utumiaji mabavu za makundi yenye uhusiano na mitandao ya kigaidi ya Al Qaeda na DAESH (ISIS).

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyojiri mwaka 2020 na 2021; na kutokana na utashi wa baraza la kijeshi linalotawala wa kutaka kuendelea kubaki madarakani kwa miaka kadhaa, kuanzia mwezi Januari mwaka huu nchi hiyo iliwekewa vikwazo vikali vya kiuchumi na kidiplomasia hasa vya Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.

Mgogoro wa hali mbaya ya kiusalama umeigubika Mali tangu mwaka 2012; na vikosi vya majeshi kutoka nje hasa vya Ufaransa havijaweza kurejesha amani na usalama katika nchi hiyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live