Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burundi yatuma kikosi cha waokoaji UturukiJumapili, Februari 12, 2023

Tetemeko La Ardhi Uturuki Na Syria Laua Watu Zaidi Ya 5,000 Burundi yatuma kikosi cha waokoaji UturukiJumapili, Februari 12, 2023

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lilioikumba nchi za Syria na Uturuki lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 28,000 na uharibifu mkubwa, Serikali ya Burundi imeamua kutuma timu ya watu 10 kwenda kusaidia uokoaji.

 Hii imekuja kama hatua ya mshikamano na watu wa Uturuki waliokumbwa na matetemeko makubwa ya ardhi tangu Jumatatu na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha.

"Wakati wa kuwasili, timu itatumwa na mamlaka ya Uturuki katika maeneo ambayo wanaihitaji zaidi," amesema Albert Shingiro, waziri wa mambo ya nje wa Burundi ameliambia shirika la habari la BBC siku ya Jumapili.

Shingiro amesema,“hakuna raia wa Burundi aliyeathiriwa, na Sabria Samir Kaze ambaye alikuwa katika mji wa Gaziantep, uliokumbwa vibaya na tetemeko la kwanza alihamishwa hadi Ankara.”

Burundi haikutuma waokoaji Syria kwa sababu ni vigumu kufikia maeneo yaliyoathiriwa hata hivyo, serikali inasema inawahurumia watu wanaoteseka huko nchini Syria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live