Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burundi yapata shavu, yapewa hekta 10 kujenga bandari kavu Tanzania

Burundi Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Gabriel Migire, Katibu Mkuu Wizara ya Biashara Burundi Jere

Mon, 30 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipatia eneo la hekta kumi Serikali ya Burundi kwa ajili ya kujenga Bandari kavu eneo la Kwala, mkoani Pwani. Lengo la ujenzi huo ni kurahisisha shughuli za kibiashara zinazohusisha uchukuzi wa bidhaa muhimu baina ya nchi hizo mbili.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Burundi nchini Tanzania Bw. Gervais Abayeho,na kuongeza kuwa kupatikana kwa eneo hilo kutasaidia wafanyabishara wa Burundi kuweza kuhifadhi shehena zao kabla ya kusafirisha kwenda Burundi , na hivyo kusaidia kupunguza gharama za utunzaji wa mizigo yao wanazozipata kwa sasa.

“Nichukue fursa hii kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kutupatia eneo hili kwa ajili ya ujenzi wa Bandari Kavu, tunaamini upatikanaji wake utakuwa mkombozi kwa wasafirishaji wetu”, amesema Balozi Abayeho.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt.Leonard Chamuriho, amemhakikishia Balozi huyo pamoja na Ujumbe aliokuja nao kutoka nchini Burundi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaama na kupeleka nhini humo ili kukuza mahusiano mazuri ya kibiashra.

Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt. Jilly Maleko, kwa upande wake, amesema upatikanaji wa eneo hilo la Bandari kavu kutapelekea wafanyabiashara wa Burundi kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa kiwango kikubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live