Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burundi yaamuru kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani

Burundi Pic Sylvester Nyandwi, kiongozi wa upinzani Burundi

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Burundi imetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani nchini humo, Alexis Sinduhije aliye uhamishoni nchini Ubelgiji kwa tuhuma za kuongoza kundi la kigaidi ambalo linatuhumiwa kufanya vitendo vingi vya kigaidi katika taifa hilo.

Taarifa hii imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa serikali , Sylvester Nyandwi kufuatia mfululizo wa matukio ya kutishia amani yanayoendelea kutekelezwa na kikundi hicho kinachofahamika kwa jina la 'Red Tabara'.

Mwanasheria huyo ameongeza kusema kuwa, matukio mengi ya kigaidi yaliyotokea mwaka 2020 yalifanywa na kundi hio linalo ongozwa na kiongozi huyo.

"Uchunguzi umeshafanyika, na tumebaini kuwa matendo haya yamefanywa na kundi hilo la kigaidi linaloongozwa na Alexis Sinduhije.

"Kwa mujibu wa sheria ya nchi na ile ya kimataifa, vitendo hivi ni kinyume na Katiba, pia vipo kinyume na misingi ya haki za binadamu" amesema Mwanasheria huyo.

Kwa miaka mingi Serikali ya nchini humo imekuwa ikimtuhumu kiongozi huyo kuwa anaongoza kundi hilo hatari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live