Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burundi nchi ya pili kwa umasikini Duniani

Burundi Msjsal Burundi nchi ya pili kwa umasikini Duniani

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mjibu wa Global Finance, Burundi imewekwa nafasi ya pili kwa umaskini Duniani huku pato la raia likiwa ni wastani wa dola 890 kwa mwaka.

Burundi ni nchi ndogo isiyo na Bahari na imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 12 na kuchangia katika orodha ya nchi ya pili maskini zaidi duniani, huku takriban asilimia 80 ya wananchi wake wapatao milioni 13 wakitegemea Kilimo kwa kujikimu.

Mfumuko wa bei ukikadiriwa mwaka huu kuwa karibu 16%.

Rais Evariste Ndayishimiye amefanya jitihada za kuinua upya uchumi na kurekebisha uhusiano wa Kidiplomasia na mwaka 2022 Marekani na Umoja wa Ulaya zilianza tena kutoa msaada baada ya kuondoa vikwazo vya kifedha.

Kwasasa, Sudani Kusini ndiyo nchi ya kwanza kwa umaskini Duniani wastani wa dola 476 kwa raia kwa mwaka mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live