Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burundi kunufaika na mradi wa ajira

033fab90f6fad8c3b2fef9b2db210616 Burundi kunufaika na mradi wa ajira

Tue, 15 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BURUNDI imejumuishwa katika mradi wa majaribio na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ulioundwa kusaidia kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana katika eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mradi huo wa miaka miwili, ni wa kwanza kufadhiliwa na AfDB nchini Burundi na utasaidia vijana na sekta binafsi katika ubunifu wa miradi ili kuongeza ajira.

"Mradi huu unakusudia kuunganisha ustadi katika maendeleo ya jumla ya Burundi, ikisisitiza uhamishaji wa maarifa na kubadilishana uzoefu wa aina zote," alisema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Maendeleo, Balozi Albert Shingiro.

Mradi huo unalenga kukusanya wataalamu 450 kutoka Uganda na Burundi ambao ni vijana kutoka sekta binafsi na umma kwa ajili ya maendeleo ya kwenye sekta ya uchumi na kuibua fursa mbalimbali nchini Burundi ambazo zitatambuliwa kupitia utafiti wa soko.

Majaribio hayo yataanza na tathmini ya mahitaji na utafiti wa masoko kuhusu fursa zinazojitokeza katika majimbo mawili yaliyolengwa nchini Burundi.

Mradi huo unakadiria kuanza na angalau vijana 450 kwa kuwapatia mafunzo na watakaochaguliwa watasaidiwa kuanzisha biashara ndogo na za kati katika nyanja mbalimbali.

Mwakilishi wa AfDB, Abdoulaye Konaté, alisema mradi huo ni sehemu ya mpango mkakati wa vijana barani Afrika (2016-25), kwa lengo la kukuza ukuaji wa uchumi na kuunda ajira milioni 25 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na kuwapa vijana milioni 50 ujuzi wa kutoa ajira ndani ya miaka 10 (2016-2025).

Chanzo: habarileo.co.tz