Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burundi: Waziri Mkuu wa zamani afikishwa mahakamani

Waziri Mkuu Zamani Burundi Waziri Mkuu wa zamani afikishwa mahakamani

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa zamani wa Burundi, Alain-Guillaume Bunyoni, amefikishwa mahakamani siku ya Alkhamisi, akituhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa na kumtusi rais.

Alain-Guillaume Bunyoni, ambaye alikuwa Waziri Mkuu tangu mwezi Juni 2020, alifutwa kazi mnamo mwezi Septemba 2022, siku chache baada ya rais Evariste Ndayishimiye kushutumu majaribio ya "mapinduzi ya serikali". Nafasi yake ilichukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Gervais Ndirakobuca.

Kwa muda mrefu Bwana Bunyoni alikuwa akichukuliwa kuwa ndiye kiongozi nambari mbili wa kweli wa utawala na kiongozi wa watu wenye msimamo mkali kati ya majenerali wanaoshikilia madaraka. Alikamatwa mwezi Aprili mwaka huu katika mji mkuu wa kiuchumi Bujumbura, na tangu wakati huo anazuiliwa katika mji mkuu Gitega. Kesi ilianza mbele ya Mahakama ya Juu, ambayo ilisikizwa gerezani. Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi

"Jenerali Bunyoni alionekana na washtakiwa wenzake sita katika chumba kilichokarabatiwa vizuri katika gereza kuu la Gitega, asubuhi ya Alhamisi kuanzia saa tano mchana hadi saa saba, mbele ya karibu watu hamsini akiwemo mmoja wa binti zake," chanzo cha mahakama ambacho kimeombwa kutotajwa jina kimeliambia duru za habari.

Walioshuhudia wanasema, alikuwa amevalia sare ya kijani kibichi ambazo ni nguo wanazovaa wafungwa nchini Burundi. Kulingana na chanzo cha mahakama, alishutumu "mazingira mabaya" ya kuzuiliwa kwake.

Ulinzi ulikuwa mkali ndani ya gereza hilo na pia kwa watu wote walioingia ndani ya chumba cha mahakama wakiwemo waandishi wa habari hawakuruhusiwa kubeba kalamu, miwani, simu wala kamera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live