Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burundi: Watu 20 wauawa shambulio la waasi

Waasi Shambulio Burundi: Watu 20 wauawa shambulio la waasi

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Burundi imetangaza kuwa, watu 20, wakiwemo wanawake na watoto wadogo, wameuawa katika shambulizi la kundi la waasi waliokuwa na silaha magharibi mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Burundi imesema mauaji hayo yametekelezwa na waasi wa RED-Tabara, ambao katika taarifa yao iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X, wamesema wamewauwa wanajeshi 10 wa serikali.

Msemaji wa serikali ya Burundi, Jerome Niyonzima, amesema kuwa shambulio hilo lilitokea Ijumaa usiku katika kijiji cha Vugizo kulichoko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Watoto 12 na wanawake wawili wajawazito ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo.

Serikali ya Burundi imelitaja shambulio hilo kuwa la kigaidi.

Hilo ni shambulio ya pili ndani ya wiki mbili kutekelezwa na waasi hao, ambao tangu Septemba mwaka 2021, wameendelea kuitatiza serikali ya Burundi.

Tangu kuundwa kwake mwaka 2011, kundi la RED-Tabara, lenye wanachama karibu elfu moja limeteleza mashambulio kadhaa nchini Burundi.

Kundi hili la RED-Tabara linatambuliwa kuwa genge kuu lenye silaha linalopigana na serikali ya Rais Evariste Ndayishimiye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live