Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burundi, Misri zakubaliana mambo matano

40d6ba0e4bea1c609c37645b09080fe7 Burundi, Misri zakubaliana mambo matano

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BURUNDI na Misri zimesaini hati za makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya utalii, elimu, utamaduni, mawasiliano pamoja na msamaha wa viza.

Taarifa kutoka mtandao wa twitter wa Rais wa Burundi imeeleza kuwa, makubaliano hayo pia yanayohusu masuala ya pasipoti za kidplomasia na huduma nyingine za utekelezaji wa rasilimali za maji nchini..

Ilieleza kuwa ujumbe wa Burundi na Misri chini ya uongozi wa wakuu wa nchi hizo walifanya majadiliano kuhusu uwekezaji, teknolojia, miradi katika Ziwa Tanganyika, pamoja na misaada ya Misri katika sekta za miundombinu na afya.

Ujumbe wa Burundi ulihusisha mawaziri wanne, Mkuu wa Diplomasia, Albert Shingiro, Waziri wa Afya Thaddée Ndikumana, Waziri wa Kilimo na Mifugo, Déo-Guide Rurema na Waziri wa Nishati na Madini, Ibrahim Uwizeye.

Rais Evariste Ndayishimiye alianza ziara rasmi nchini Misri Machi 23 hadi Machi 26, mwaka huu na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri, Abdel Fattah Al-Sissi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz