Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burkina Faso na Niger zajiondoa katika Kikosi cha G5 Sahel

5H Sahel.jpeg Burkina Faso na Niger zajiondoa katika Kikosi cha G5 Sahel

Sun, 3 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Burkina Faso na Niger, nchi mbili zinazoongozwa na majeshi yaliyotwaa madaraka kupitia mapinduzi, jana Jumamosi zilitangaza kwamba zimejiondoa katika kikosi cha pamoja kwa jina la G5 Sahel kinachopambana dhidi ya makundi ya wanamgambo wenye silaha, zikijiungana na jirani yao Mali, iliyojiondoa katika kikosi hiki mwezi Mei mwaka jana.

Nchi hizo mbili zimeamua kwa mamlaka kamili kujiondoa katika taasisi zote za G5 Sahel, pamoja na Kikosi cha Pamoja cha kupambana na makundi ya wanamgambo wenye silaha", tangu Novemba 29 mwaka huu.

Kundi hili tajwa liliundwa mwaka 2014 kwa lengo la kupambana dhidi ya makundi ya wanamgambo wenye silaha katika eneo la Sahel barani Afrika Sahel, kwa kuzijumuisha Mali, Burkina, Niger, Mauritania na Chad.

Wanamgambo wenye silaha huko Mali Burkina faso na Niger zimesema katika taarifa yao kuwa Jumuiya hii imeshindwa kufikia malengo yake na kwamba kundi la G5 Sahel haliwezi kutumikia maslahi ya nchi ajinabi kwa kuharibu na kuvuruga maslahi ya watu wa eneo la nchi za Sahel.

Nchi tano yaani Mali, Burkina Faso, Niger,Mauritania na Chad ziliunda kundi la G5 Sahel mwaka 2014 na kisha ziliasisi jeshi lake mwaka 2017 wakati wanamgambo wanaobeba silaha walipokuwa wakiimarisha ngome zao katika nchi hizo .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live