Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burkina Faso kutia saini mkataba wa nishati ya nyuklia na Urusi

Burkina Faso Kutia Saini Mkataba Wa Nishati Ya Nyuklia Na Urusi Burkina Faso kutia saini mkataba wa nishati ya nyuklia na Urusi

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Burkina Faso na Urusi zimeratibiwa kutia saini mkataba wa maelewano (MoU) kwa ajili ya ujenzi wa kinu cha nyuklia katika taifa hilo la Afrika Magharibi, kulingana na shirika la habari la serikali la AIB.

Makubaliano hayo yatakuwa kilele cha mazungumzo ya mtawala wa kijeshi wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traoré, na Rais wa Urusi Vladimir Putin mwezi Julai, wakati wa mkutano wa kilele wa Urusi na Afrika mjini Moscow.

"MoU itatiwa saini kati ya Rosatom, wakala wa shirikisho wa nishati ya atomiki ya Urusi, na wizara ya nishati ya Burkina Faso, pembezoni mwa Wiki ya Nishati ya Urusi 2023," AIB ilisema.

Takriban 20% ya wakazi wa Burkina Faso wanapata umeme - ikiwa ni ya viwango vya chini zaidi duniani, kulingana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA).

Baada ya kutofautiana na washirika wake wa jadi wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Burkina Faso imegeukia Urusi kwa msaada wa kiuchumi na kijeshi.

Chanzo: Bbc