Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burkina Faso kupeleka wanajeshi Niger

Niqer Tishio Nigeria.jpeg Burkina Faso kupeleka wanajeshi Niger

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza kusema Baraza la Mawaziri nchini Burkina Faso, ni kama limewasha taa ya kijani ambayo inairuhusu Serikali ya nchi hiyo, kupeleka wanajeshi wake Niger, ili kusaidia masuala mazima ya ulinzi na usalama nchini humo.

Hatua hii pia inatizamwa kama njia ya kuimalisha usalama wa Burkna Faso, ambao ni majirani na Niger, nchi ambayo jeshi lilimwondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum takriban mwezi mmoja uliopita.

Mtandao wa AA umeandika kuwa, taarifa ya Baraza la Mawaziri Jumatano jioni imesema, “kutokana na mipango ya kimkakati ya nchi yetu," Serikali imeruhusiwa kupeleka kikosi cha kijeshi nchini Niger.

"Bila ya kuchochea vita, ni lazima ieleweke kwamba jambo hili lifanyika kwa kuwa ni wajibu wetu kuzuia, na kwa maslahi bora ya mapambano yetu dhidi ya ugaidi, na haya ndiyo matarajio makubwa ya watu wa Burkinabe," amesema Waziri wa Ulinzi Kanali Meja Kassoum Coulibaly, na kuongeza;

"Kinachoathiri usalama wa Niger kimsingi kinaathiri usalama wa Burkina Faso."

Wiki iliyopita, utawala wa kijeshi wa Niger uliidhinisha wanajeshi kutoka nchi jirani za Mali na Burkina Faso kuunda jeshi moja la Niger iwapo kutatokea uvamizi wa kijeshi.

Vitisho hivyo, vilikuwa vimetolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas), kwamba ingetuma vikosi vyake iwapo wanajeshi hao hawatarejesha utawala wa kiraia wa Rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum.

Niger ilitumbukia katika machafuko Julai 26 wakati Jenerali Abdourahamane Tchiani, kamanda wa zamani wa walinzi wa Rais, alipoongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa Rais Bazoum.

Wanajeshi wa Burkina Faso na Mali wametangaza kuungaji mkono utawala wa kijeshi nchini Niger.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live